EVANS Aveva amechaguliwa kwa kishindo kuiongoza Simba katika
uchaguzi mkuu uliofanyika jijini Dar es Salaam jana, huku mashabiki na
wanachama wa Msimbazi wakiimba kwa furaha kwamba wamempata rais kiboko
ya Yanga na kocha wao mpya, Marcio Maximo ‘The Chosen One’.
Aveva katika kampeni zake aliweka bayana na hata jana alisisitiza kwamba wanachama wamkabidhi uongozi aimalize Yanga.
Matokeo ya awali kwa mujibu wa watu waliokuwa
chumba cha kuhesabia kura Aveva amepata 1452 huku mpinzani wake Andrew
Tupa akipata kura 386 na kura sita zikiwa zimeharibika.
Kwa Makamu wa Rais, hadi tunakwenda mitamboni
Geofrey Nyange ‘Kaburu’ alikuwa amewashinda Swedy Mkwabi, Jamhuri
Kihwelo ‘Julio’ na Bundala Kabulwa. Kura za wajumbe zilikuwa
zinaendelea kuhesabiwa.
Kwa wajumbe hadi tunakwenda mitamboni washindi walikuwa ni Said Tully, Idd Kajuna, Jasmin Sudi na Collins Frisch.
0 comments:
Chapisha Maoni