Aliyekuwa kaimu kocha na Mchezaji wa Manchester United Ryan Giggs
amekiri kuwa hakuwa tayari kwa majukumu ya kazi kama kocha wa klabu hiyo
ya Uingereza.Giggs anasema kuwa uteuzi huo ulikuwa mapema kuliko
alivyotarajia.
Giggs alichukua hatamu kama kaimu kocha mwisho wa
msimu uliopita baada ya kocha David moyes Kutemwa kufuatia msururu wa
matokeo duni tangu achukue hatamu Old Trafford.Giggs aliyekuwa kocha
katika mechi nne za mwisho alitwaa ushindi katika mechi 1 akashindwa
moja na kisha akatoka sare katika mechi ya mwisho Manchester united
ilipomaliza msimu katika nafasi ya 7 .
0 comments:
Chapisha Maoni