Hakika chaguzi hizi zinazofuata, zitawarudisha Wasakatonge na
Intarahamwe wengi vijijini kwao kutoka Dar Es Salaam, hatutakuwa na cha
swalia mtume kwamba alikopa Benki za Umma wa Watanzania mamillioni ya
Shillingi, mali zake zote zitapigwa mnada, zikawasaidie Wanafunzi
wanaoketi juu ya mawe na akina mama wajawazito wanaojifungulia sakafuni kwa kukosa vitanda mahospitalinl huko majimboni.
Ikumbukwe kwamba Chadema ni Chama Kikuu cha upinzani Nchini, hatua ya
kuitwa Chama Kikuu Cha upinzani Nchini ni 'Long Process' inayopitia
matukio mengi ambayo sio kirahisi tu kuishushia hadhi Chadema kwa
matumizi ya 'Poor technics' kama hizi tunazoshudia sasa. Sisi hatuna
wasiwasi hata kidogo kwa sababu hawa ni watu wadogo sana.
Endeleeni kuzitangaza Ilani, Falsafa, Sera na Itikadi za Chama chetu
kama kawaida popote pale mlipo, hizi ni dalili za wazi za anguko la
watawala wanaoamini kabisa kwamba uongozi wa kidemokrasia ni mtaji wa
maisha ya mhusika.
0 comments:
Chapisha Maoni