Jumapili, Juni 29, 2014

ALICHOKISEMA DIAMOND PLATNUMZ BAADA YA KUKOSA TUZO BET 2014!

Muda mfupi baada ya mshindi wa tuzo ya BET 2014 kwa wasanii wa Afrika kutangazwa kuwa Davido wa Nigeria, staa kutoka Tanzania Diamond Platnumz aliekua anawania pia tuzo hiyo ameandika katika mtandao wa kijamii wa Instagram na ni ujumbe maalumu kwa mashabiki wake na watanzania wote:
Tusipopenda kukubali matokeo na ushindi wa wenzetu basi daima hatutaweza kuwa washindani, muhimu ni kujua wapi tulipotoka na wapi tulipo leo, katika nchi zaidi ya 20 zenye wasanii zaidi ya milioni 40 kuchaguliwa Tanzania ni fursa, heshima na hatua kubwa, cha muhimu ni kuitumia vyema fursa hii na kuhakikisha mwakani tunapiga hatua, asante sana kwa wote wanaozidi kunisupport

0 comments:

Chapisha Maoni