Jumapili, Juni 29, 2014

DIDA AMFUMANIA MUMEWE, WAACHANA

Kutoka kwa chanzo chetu makini na wakuaminika alieomba hifadhi ya jina lake ametueleza kuwa ndoa ya Dida haipo tena baada ya Dida kumfumania mumewe na dogo dogo. Chanzo hicho kimedai kuwa Dida alimfumania mume wake ambae ni mtangazaji Ezden Jumanne na ndoa imevunjika rasmi na Ezden Jumanne amepokonywa vitu vyote vya thamani alivyokua amepewa na Dida,kama gari,simu ya thamani na vingine.
We yaani ulitokea ugomvi mkubwa balaa yaani nusu afe mtu,mbona kitaa kilikua kazi ! kipindi kile ilifunga kwa kigodoro sasa safari ilifunga kwa fumanizi. Hii ni ndoa ya 3 kwa mwana dada huyo ambae aliwahi kusema kua na hii ikivunjika basi hata kaa aolewe tena,waswahili wanasema usitukane mamba kabla hujavuka mto, tayari bidada kashavunja ndoa 3 na kumfanya awe katika rekodi ya aina yake hapa mjini kwa umri alionao na idadi ya ndoa alizopitia.
Nina mwonea huruma yule Ezden maskini hana kitu ni wale wakaka wanaolelewa hapa mjini,yaani ye alikua anavishwa,analishwa na pesa ya kutumia inatoka kwa mamaa Dida,chezea Dida wewe
Kiliongeza Chanzo chetu.

0 comments:

Chapisha Maoni