Maafisa wa kijeshi wa Cameroon wamesema kuwa, wamewatia mbaroni
wafanyabiashara 50 wa Nigeria kwa madai ya kushirikiana na kundi la Boko
Haram huku wanajeshi wa Cameroon wakiripotiwa kuuwa wanamgambo 10 wa
kundi hilo.
Mtandao wa gazeti maarufu la Punch la nchini Nigeria umeripoti habari hiyo leo na kuongeza kuwa, wafanyabiashara hao wa Nigeria wametiwa mbaroni katika eneo la Mora kwenye mpaka wa Cameroon na jimbo la Borno la Nigeria.
Msemaji wa jeshi la Cameroon, Kanali Chioka Pierre amesema kuwa, jeshi la nchi yake limeua wanamgambo kadhaa wa Boko Haram na kuteka magari kadhaa pamoja na kiwango kikubwa cha silaha sambamba na kuwatia mbaroni makumi ya watu kwa tuhuma za kuwa na uhusiano na kundi hilo.
Cameroon imeweka maelfu ya askari wake katika mpaka wake wa pamoja na Nigeria hususan kwenye maeneo ya Cameroon yanayopakana na jimbo la Borno ambalo linahesabiwa kuwa kitovu cha kundi la Boko Haram huko Nigeria.

0 comments:
Chapisha Maoni