Watu nchini India wameghadhabishwa na uzembe wa
polisi katika jimbo la Uttar Pradesh kufuatia tukio la wasichana wawili
kubakwa na kuuawa na mili yao kuwekwa juu ya mti.
Babake mmoja wa wasichana hao amesema kuwa
polisi walimkejeli alipokwenda kwao kutaka usaidizi wa kumtafuta
msichana wake aliyetoweka kabla ya kupatikana akining'inia kwenye mti na
mwenzake.
Alisema kuwa wakati polisi
walipogundua kuwa anatoka katika tabaka linalotazamiwa kuwa la hadhi ya
chini, walikataa kumsaidia kutafuta msichana wake.
Watu watatu akiwemo polisi mmoja wamekamatwa kuhusiana na tukio hilo.
Familia za waathiriwa zimelalamika kwamba polisi
walikataa kuwasaidia kutafuta wasichana hao waliokuwa na umri wa miaka
14 na 16 mtawalia na ambao pia wanatoka familia moja.
nilipokwenda kwa polisi, kitu cha kwanza nilipoulizwa ni tabaka langu , nilipowaambia wakaanza kunitukana
alisema baba huyo wa mmoja wa wasichana hao waliobakwa kisha kuuawa.
Polisi walisema kuwa wanaume hao walikamatwa kwa kuwabaka kisha kuwaua wasichana hao.
Polisi mmoja pia alizuiliwa kwa kushirikiana na
washukiwa na pia kwa kukosa kuchukua hatua. Bado mshukiwa mmoja anasakwa
na polisi.
0 comments:
Chapisha Maoni