Ijumaa, Mei 30, 2014

MREMBO WA CHUO KIKUU UDSM AFARIKI DUNIA AKIWA USINGIZINI

Mwili wa mwanafunzi wa UDSM baada ya kufariki akiwa amepumzika
Taarifa za kusikitisha sana! Ni tukio ambalo limeshangaza na kushtua kupita kiasi baada ya mwanafunzi wa chuo kikuu cha UDSM mkoani Dar es Salaam kufariki dunia ghafla mchana wa leo. Inasemekana kwamba mwanafunzi huyo ambaye jina lake halikufahamika mara moja ni wa mwaka wa pili.
Taarifa za awali zinasema kwamba mwanafunzi huyo alikuwa akisoma na wenzake na baadae alijisikia kuchoka kitu kilichopelekea kwenda hostel kupumzika ambapo mauli yalimkuta akiwa kitandani kwake na haijafahamika chanzo cha kifo chake ni nini mpaka sasa lakini habari zikija zaidi nitakupatia, endelea kuperuzi Fichuo Tz.
Mwili wa mwanafunzi ukitolewa hostel
Mwili ukipakiwa katika gari la wagonjwa kwaajili ya uchunguzi

0 comments:

Chapisha Maoni