Ijumaa, Mei 30, 2014

FAHAMU JINSI MIKONO INAVYOAMBUKIZA MAGONJWA

Kutokana na tabia ya kuambukiza, magonjwa yanaweza kugawanywa kimsingi katika makundi makuu mawili, yaani magonjwa yasiyoambukiza au magonjwa yanayoambukiza.
Magonjwa yanayoambukiza husambaa haraka miongoni mwa jamii kupitia njia ya kugusana.
Mkurugenzi na mtaalamu wa masuala ya elimu ya maambukizi ya vimelea vya magonjwa na kinga ya mwili wa kituo cha utabibu cha Chuo Kikuu cha New York, Dk Philip Tierno anasema asilimia 80 ya magonjwa yote ya kuambukiza husambazwa kwa njia ya kugusana moja kwa moja na chanzo chenye vimelea vya ugonjwa au kwa kugusana na mtu kupitia njia ya kushikana mikono.
Historia inaonyesha kuwa desturi ya kushikana mikono ilianza zamani sana, yapata karne ya pili kabla ya kuzaliwa kwa Kristo na makusudi yake yalikuwa ni kumthibitishia usalama mtu unayekutana naye.
Katika jamii mbalimbali duniani, watu hushikana mikono mara kwa mara kwa ajili ya kusalimiana, kupongezana, kupimana nguvu, kusameheana na wengine kuonyeshana mshikamano wa kijamii.
Ingawa kushikana mikono ni jambo zuri katika kuimarisha uhusiano wa kijamii, wanasayansi wa masuala ya afya ya jamii wanaonyesha kuwa jambo hili pia linaweza kusababisha hatari za kiafya hasa wakati wa mlipuko wa magonjwa hatari yanayosambaa haraka kwa njia ya kugusana.
Dk Innocent Mosha wa Kitengo cha Uchunguzi wa Magonjwa katika  Hospitali ya Muhimbili anasema, vimelea vya maradhi vinaweza kusambaa kwa urahisi kwa kupitia mikono yetu.
 Kwa mfano anasema magonjwa  yaenezwayo na virusi kama mafua, husambaa kwa wepesi zaidi endapo watu watapeana mikono bila kuzingatia kanuni za usafi.  Pia anasema ugonjwa wa homa ya ini unaweza kuambukizwa iwapo watu watashikana mikono, hasa ikiwa mmoja wao ana damu yenye virusi vya homa hiyo au kuwa na michubuko na jeraha.
Magonjwa yanayosababishwa na vimelea vya maradhi huchangia kwa kiasi kikubwa maambukizi. Ni vyema watu wakazingatia usafi wa mikono, hasa baada ya kupenga kamasi, kupiga chafya, kutoka chooni,  kabla na baada ya kula
 anasema

0 comments:

Chapisha Maoni