Jumamosi, Mei 03, 2014

MVUA YAVURUGA SHOO YA LADY JAY DEE USIKU WA KUAMKIA LEO

MVUA kubwa iliyonyesha usiku wa kuamkia leo imetibua shoo ya mkali wa muziki wa Bongo Fleva, Lady Jay Dee nakusababisha shoo hiyo kusogezwa mbele mpaka itakapotangazwa.

Shoo hiyo iliyopangwa kufanyika katika ukumbi wa Nyumbani Lounge ambapo mbali na Lady Jay Dee walikuwa wamealikwa wasanii wengine wakiwemo, Prof. Jay, Patricia Hillary, Roma mkatoliki, Baghdady na wengine kibao.

Mvua hiyo ambayo ilianza kunyesha toka majira ya jioni na kuzua hofu ya kuendelea kwa shoo mpaka kufikia saa saba za usiku mwanadada Jide alipanda jukwaani na kuomba radhi kwa mashabiki waliokuwa wamehudhuria ukumbini hapo kutokana na hali hiyo nakuwahaidi kuwa shoo hiyo itarudiwa tena ila kwa wale waliojitokeza watapatiwa tiketi ya shoo ijayo (Hawatalipa kiingilio tena). Baada ya kuomba radhi alipiga nyimbo zake kadhaa akifuatiwa na wasanii wengine.

0 comments:

Chapisha Maoni