Familia moja iliyopo katika nyumba za CCM eneo la Sahare jijini Tanga
imenusurika kifo baada ya mti aina ya mbuyu kuangukia katika nyumba yao
na kuvunja vyumba viwili vya kulalia kufuatia mti huo kuangushwa na
mvua za masika zinazoendelea kunyeesha katika maeneo mbalimbali hapa
nchini.
Kiongozi wa familia hiyo bwana Massud Mwabumba amesema
dhoruba ya mti huo imetokea majira ya saa tano asubuhi wakati watoto
wake wawili wakiwa sebuleni na yeye akiwa chumbani ndipo alipohisi muungurumo mithili ya radi na alipokimbia nje yeye na watoto wake na kukuta mbuyu huo ukiangukiwa katika nyumba yao
Mmoja kati ya waathirika wa tukio hilo Bi.Hellen Kwingwa amesema mti
huo umevunja bimu la ukuta kisha kuangukia katika kitanda chao cha
kulalia ambacho kilivunjika vipande viwili na kuongeza kuwa endapo
tukio hilo lingetokea usiku hakuna hata mmoja katika familia yao ambaye
angenusurika kifo .
Kufuatia tukio hilo baadhi ya watu wanaoishi katika nyumba zenye mibuyu kama wa aina hiyo wameshauriwa kuchukua hatua mapema za kuikata hasa kipindi hiki cha mvua za masika kwa sababu hili ni tukio la pili , la kwanza likiwa limetokea eneo la Potwe wilayani Muheza baada ya mti wa aina hiyo kuangukia nyumba yao na kusababisha vifo vya watu wawili waliokuwa ndani ya nyumba zao .

0 comments:
Chapisha Maoni