Jumatatu, Mei 05, 2014

AKUTWA AMEFARIKI KWENYE PAGALA IRINGA

Mtu mmoja amekutwa amefariki kwenye pagale na huku watu wawili wakishikiliwa na Jeshi la polisi Mkoani Iringa kwa tuhuma tofauti ikiwepo ya ubakaji.
Akithibitisha kutokea kwa matukio hayo Kamanda wa jeshi la polisi Mkoani Iringa ACP Ramadhani Mungi amesema mtu asiyefahamika jina wala makazi yake jinsia ya kiume umri kati ya miaka 40 amekutwa amefariki eneo la Frelimo A kata ya Makorongoni Mkoa na Manispaa ya Iringa.
Ameongeza kuwa Jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi zaidi wa chanzo cha tukio hilo ambapo mwili wa marehemu umekutwa kwenye pagare la nyumba ambayo hawaishi watu.
Kamanda Mungi amesema katika tukio la pili,Musa Mgowa mwenye umri wa miaka 45 mkazi wa kijiji cha Matalawe Wiyaya ya Kilolo Mkoa wa Iringa anashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma ya kumlawiti motto wa miaka 4 na kumsababishia maumivu makali.
Wakati huo huo, amesema Adanu Lunyungu mwenye umri wa miaka 19 mkazi wa Kijiji cha Ilambilole Kata ya Isimani Wilaya ya Iringa Vijijini Mkoani Iringa anashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma ya kumbaka mwanafunzi wa awali mwenye umri wa miaka 5.
Hata hivyo Kamanda Mungi amesema taratibu za kisheria zinaendelea kufuatwa ili watuhumiwa waweze kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili mara baada ya uchunguzi kukamilika.

0 comments:

Chapisha Maoni