IMANI ya kuabudu inayotiliwa shaka duniani ya Freemason imetajwa kuwa
nyuma ya pazia la ajali mbaya ya Basi la Sumry iliyotokea katika Kijiji
cha Ulyampiti mkoani Singida mwanzoni mwa wiki iliyopita na kusababisha
vifo vya watu 19, wakiwemo polisi wa usalama barabarani wanne.
Habari za uhakika kutoka kijijini hapo zinasema siku moja baada ya
ajali hiyo mbaya, basi moja linalosafiri kati ya miji ya Bukoba na Dar
es Salaam (jina linahifadhiwa) lilipita katika kijiji hicho na kutupa
karatasi zilizokuwa na maneno ya kuwahamasisha watu kujiunga na dini
hiyo inayodaiwa kuwa ya kishetani.
Inadaiwa kuwa kwenye karatasi hizo kulikuwa na mchoro unaoaminika
kutumiwa na watu wa dini hiyo ambapo pia ilichorwa michoro yenye
kuonesha burungutu la fedha, sanjari na namba za simu zinazowataka watu
kuzitumia endapo watataka kujiunga.
Tulipoziona zile karatasi na kuzisoma, wengi tulikimbia kwa sababu tunahusisha kabisa na ajali ya Sumry. Mbaya zaidi ajali yenyewe inatia shaka. Mimi nilipoambiwa kuhusu hizo karatasi, sikutaka kuziona, nikakimbia
alisema mwanamke mmoja aliyejitambulisha kwa jina la
Yasinta, mkazi wa kijiji hicho.
Alisema karatasi hizo zilitupwa pia katika Vijiji vya Isuna, Nkuhi, Samumba na Ikungi wakati basi hilo ambalo mara kwa mara huripotiwa kupata ajali, likiwa katika safari yake kuelekea Dar es Salaam.
Alisema karatasi hizo zilitupwa pia katika Vijiji vya Isuna, Nkuhi, Samumba na Ikungi wakati basi hilo ambalo mara kwa mara huripotiwa kupata ajali, likiwa katika safari yake kuelekea Dar es Salaam.
Kijana mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Zuberi ambaye hufanya
shughuli zake katika stendi ya mabasi Kijiji cha Ulyampiti alithibitisha
kutupwa kwa karatasi hizo na yeye alikuwa nayo mkononi.
Ni kweli hizo karatasi zimetupwa, hata washikaji wa vijiji vya jirani nao wametuambia wameokota, mimi mwenyewe hapa nilipo ninayo, ina namba za simu ambazo wanasema tuwasiliane nao kama tunataka kujiunga
alisema kijana huyo na kutaja namba hizo, ambazo hata hivyo haziwezi
kuandikwa mtandaoni kwa sababu maalum.
Wanakijiji hao walikwenda mbali zaidi na kudai kuwa basi lilitupa
karatasi hizo pia limechorwa alama inayodaiwa kutumiwa na watu wa imani
hiyo katika moja ya sehemu za gari hilo ambalo hata hivyo, gazeti letu
linaendelea kufuatilia kwa karibu sakata hilo ili kujiridhisha.
Ajali ya Basi la Sumry ilitokea Jumatatu iliyopita majira ya usiku,
baada ya gari hilo kuacha njia na kulifuata kundi la watu lililokuwa
pembeni likishuhudia askari polisi wakiuchukua mwili wa mtu mmoja
aliyegongwa na gari akiwa katika pikipiki.
Inadaiwa kuwa kipande ambacho ajali hiyo imetokea kimekuwa na matukio
mengi ya kushangaza, kwani mara nyingi zinatokea ajali za kushangaza
ambazo katika kipindi cha miaka minne sasa, watu zaidi ya 50 wamepoteza
maisha katika maeneo ya jirani ya vijiji hivyo.
0 comments:
Chapisha Maoni