WAKATI akisubiri kuapishwa baada ya kuchaguliwa kwa kishindo Machi 16, mwaka huu, mbunge mteule wa jimbo la Kalenga, Godfrey Mgimwa amefanya ziara ya kuwashukuru wananchi katika baadhi ya kata za jimbo hilo pamboja na kuanza kutekeleza ahadi mbalimbali alizo ahidi jimboni humo.
Katika ziara hiyo aliyofanya katika vijiji vya Tanangozi, Kiwere, Itagutwa, Ibumilwa, Katenge na Mgama, Mgimwa alianza kutekeleza baadhi ya ahadi alizo ahidi miongoni zikiwemo zile zilizoahidiwa na aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, marehemu Dk William Mgimwa.Miongoni mwa utekelezaji wa ahidi hizo ni pamoja na kutoa bati 80 zenye thamani ya Sh 1,400,000 kwa ajili ya ujenzi wa shule ya msingi Kiwere na bati 50 zenye thamani ya Sh.875,000 kwa uongozi wa shule ya msingi Itagutwa Shule nyingine iliyonufaika na msaada kutoka kwa mbunge huyo ni shule ya msingi Makota aliyoipatia bati 50 huku akiahidi kuitembelea shule ya msingi Ugwachanya iliyochoka miundombinu yake ili kuiwekea mkakati wa kuisaidia.
Pamoja na misaada hiyo, Mgimwa ametoa ahadi ya bati 100 kwa ajili ya Shule ya Sekondari Tanangozi ambayo wanakijiji wameanza harakati za ujenzi wakiwa wameshaandaa tofari, mawe na mchanga ili kufanikisha ujenzi huo pia ametoa mifuko 30 ya sementi yenye thamani ya Sh 435,000 kwa ajili ya ujenzi wa choo cha shule ya msingi Ibumila akiwa katika kata ya Mgama.
Katika kuboresha huduma za afya kijiji hicho cha Ibumila, ameahidi kutoa Sh Milioni 2 zitakazosaidia kumalizia ujenzi wa Zahanati ya kijiji.
Hata hivyo,Mbunge mteule Mgimwa ametoa misaada mingine mbalimbali iliyolenga elimu na afya katika kuisaidia jamii jimboni humo yenye tahamani ya zaidi ya shilingi milioni nne katika kijiji cha mgama,isupilo pamoja na kijiji cha muwimbi.

0 comments:
Chapisha Maoni