Mapigano makali yamekuwa yakiendelea katika mji wa
Bentiu nchini Sudan Kusini ambapo vikosi vya serikali vinajaribu
kuurejesha mji huo uliotekwa na waasi.
Wanajeshi wa Sudan Kusini |
Mwandishi wa Habari wa BBC aliyeandamana na
kikosi cha Umoja wa Mataifa nje ya mji huo anasema amesikia milio ya
bunduki na silaha nzito nzito ambapo pia ameona kikosi cha majeshi ya
serikali kikijipanga.
Hata hivyo amesema bado haijajulikana ni kundi gani kwa sasa linaloshikilia mji huo wa wenye utajiri wa mafuta.
Kwa upande serikali nchini Sudan kusini inasema majeshi yake yameudhibiti mji wa huo na ngome ya waasi ya Nasir.
Wakimbizi baada ya machafuko nchini Sudan Kusini |
Mjumbe wa Umoja wa mataifa mjini humo anasema mji huo umedhibitiwa
upya na kikosi cha serikali katika operesheni kubwa iliyoanza hapo jana
Jumapili.
Shambulio hilo linajiri siku mbili baada ya rais
Salva Kiir kumwambia Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani John Kerry,
kwamba yupo tayari kufanya mazungumzo ya amani ya moja kwa moja na
kiongozi wa waasi, Riek Machar.
0 comments:
Chapisha Maoni