Jumatano, Mei 07, 2014

MBUNGE WA CHADEMA, LETICIA NYERERE AISHUKURU CCM

Mbunge wa Viti Maalum, Leticia Nyerere (CHADEMA), ameishukuru serikali ya CCM kwa kutekeleza miradi ya maendeleo kwa ufanisi wa hali ya juu. Nyerere amesema serikali ya CCM inapaswa kushukuriwa na kupongezwa kwani imepeleka madaktari, walimu, na imejenga barabara kila alipoomba ifanye hivyo.
Aidha, amewaomba Waziri Mkuu, mawaziri wote pamoja na Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya na viongozi wengine waendelee kumvumilia pale atakapowasumbua akiomba kero yoyote itatuliwe kwenye wilaya na jimbo lake.

0 comments:

Chapisha Maoni