Alhamisi, Mei 08, 2014

MAMBA WA BWAWA LA MTERA SASA RUKSA KUVUNWA

Wizara ya maliasili na Utalii, imetoa ruhusa ya kuvuna mamba katika bwawa la Mtera lililopo Wilaya ya Iringa Vijijini,Mkoani Iringa baada ya vifo vya wavuvi kutokea mara kwa mara.
Vifo hivyo vimetokana na kuwepo kwa idadi kubwa ya mamba katika bwawa hilo na imekuwa tishio kwa wakazi hao ambapo hadi hivi sasa idadi ya watu wane (4) wameuwawa na mamba kwa kipindi cha mwezi January hadi kufikia mwezi May mwaka huu.
Kwa upande wa ,Afisa wa Wanyama Pori na Maliasili Mkoani Iringa Bi.Rachel Muhambo, amesema kuwa katika zoezi hilo wameshafanikiwa kuwauwa mamba wawili waliokuwa tishio zaidi kwa wananchi hao.
Bi.Muhando ameongeza kuwa kwa mwaka 2012 jumla ya Mamba 20, waliuliwa katika Bwawa la Mtera huku wizara ikisitisha vibali vya uvunaji kwa Makampuni mbalimbali ambapo viboko walikuwa na utaratibu mgumu wa kuvunwa.
Hata hivyo Afisa huyo wa wanyama pori amewataka wavuvi katika bwawa hilo kuwa waangalifu, na kuhakikisha kuwa wanatoa taarifa pindi wanapowauwa mamba hao.

0 comments:

Chapisha Maoni