Hatimaye siri imefichua kuwa, ile ndoa iliyofungwa kwa mbwembwe na kuvunjika
kabla ya mwezi mmoja kati ya msanii wa filamu Tanzania, Skyner Ally
‘Skaina’ na Saad Omar, chanzo ni mwanamuziki wa bongo Fleva, Emmanuel Eribaliki
‘Nay wa Mitego’.
Habari za awali zilisema kuwa, ndoa ya Skaina iliingia mdudu baada ya
mumewe kugundua kuwa alinunua ‘mbuzi kwenye gunia’, kwani bidada huyo
alikuwa na ujauzito wa mtu mwingine.
Hata hivyo, minong’ono ilikuwa inasema kuwa, mimba hiyo ilikuwa ya Nay ingawa awali, hakuna aliyekuwa tayari kufafanua kuhusiana na ishu hiyo.
Ndoa ya wawili hao ilifungwa Oktoba 7, 2011 nyumbani kwa dada yake,
Magomeni – Mapipa, Dar na kufika tamati kabla ya mwezi Novemba.
Ripoti zilizopo zinaonesha
kuwa, baada ya Skaina kutemwa na Saad alimweleza Nay sababu na kutimkia
kwao Iringa ambapo alipojifungua alimweleza ukweli mwenzi wake huyo
kuhusu ujio wa mtoto wao.
Wawili hao wameelezwa kuwa na mawasiliano ya karibu lakini ya siri
kwa muda mrefu ila hivi karibuni, wote waliamua kuutua mzigo huo na
kuweka mambo hadharani ambapo kwa upande wa Skaina alisema:
Nadhani mmechelewa tu kujua, lakini habari ndiyo hiyo.
Nay alipoulizwa, alijibu kwa kifupi sana:
Ni kweli lakini ni mambo ambayo huwa sipendi kuyazungumzia sana.
Ili kuthibitisha ukweli huo, wikiendi iliyopita, baada ya Nay kutwaa
tuzo moja ya Kili katika kipengele cha Wimbo Bora wa Kushirikiana,
Skaina alitupia maneno ya kumpongeza Nay katika ukurasa wake kwenye
Mtandao wa Kijamii wa Instagram yaliyosema:
Hongera baba mtoto wangu kwa kuchukua tuzo, Mungu akuzidishie baraka na maisha marefu ili mwakani uweze kuchukua tuzo nyingi zaidi. Navutiwa sana na kazi zako dady wetu (akimaanisha yeye na mwanaye).
0 comments:
Chapisha Maoni