Marekani imetangaza kwamba imetuma kikosi cha
wataalamu nchini Nigeria kusaidia kuwatafuta wasichana takriban 200 wa
shule waliotekwa nyara mwezi uliopita na wapiganaji wa kundi la Boko
Haram.
Rais Barack Obama ameshutumu utekaji nyara wa
wasichana hao na kusema kuwa mataifa yanapaswa kufanya kazi kwa pamoja
ili kulikomesha Boko Haram.
Tayari tumetuma kundi letu Nigeria. Wamekubali msaada wetu ambao unashirikisha wanajeshi, wadumishaji wa sheria na mashirika mengine ambao wanajaribu kutambua waliko wasichana hawa ili wawape msaada
Rais Obama alisema.
Rais Obama amesema kuwa jamii ya kimataifa
inapaswa kutumia utekeji wa kikatili wa wasichana hao kama msingi wa
kuungana na kuangamiza Boko Haram.
Nchini Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan amekubali msaada huo kama alivyosema msemaji wake, Daktari Reuben Abati.
msaada huo kutoka kwa Rais Obama uliwasilishwa na Waziri wa Mashauri ya Kigeni John Kerry kama saa tisa alasiri hivi
Daktari Abati alisema.
0 comments:
Chapisha Maoni