Jumanne, Mei 06, 2014

MKUU WA MAJESHI MWAMUNYANGE AKEMEA WANAOIHUSISHA SIASA NA JESHI LA WANANCHI TANZANIA

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyange, amekwepa kuzungumzia au kutoa ufafanuzi kuhusu kauli zinazotolewa na baadhi ya viongozi kuwa iwapo muundo wa serikali tatu utapitishwa katika katiba mpya, Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linaweza kupindua nchi.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufungua mkutano mkuu wa nane wa Wakuu wa Idara za Ukaguzi za Majeshi (DIWG) kutoka nchi za Jumuiya ya Maendeleo za Kusini mwa Afrika (SADC), Jenerali Mwamunyange, alisema hawezi kujiingiza katika masuala ya siasa. Alitoa jibu hilo kufuatia swali la mwandishi wa NIPASHE aliyetaka kujua (CDF) anatoa kauli gani kufuatia baadhi ya viongozi wa kisiasa nchini kulihusisha jeshi hilo na siasa huku wakidai iwapo muundo wa serikali tatu ambao unalitikisa Bunge Maalum la Katiba utapita, basi, jeshi linaweza kupindua nchi.
Baadhi ya wanasiasa wamekuwa wakitoa kauli ndani na nje ya Bunge Maalum la Katiba kwamba ikiwa muundo wa serikali tatu utapitishwa kama ilivyopendekezwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jeshi linaweza kuasi na kupindua nchi ikiwa serikali ya Muungano itakosa mapato na kushindwa kuwalipa mishahara wanajeshi.
Mara ya kwanza Rais Jakaya Kikwete akizindua Bunge Maalum la Katiba alitoa kauli hiyo, akionya kuwa kuanzishwa kwa muundo wa serikali tatu kunaweza kuwa na madhara mengi kijamii, kutokana na gharama za kuziendesha.

0 comments:

Chapisha Maoni