Viongozi kumi na watatu wa mataifa na mamia ya wafanyabiashara
wanakutana Abuja kwa mkutano wa biashara na masuala ya uchumi duniani
kuhusu Afrika.
Mkutano huo mwaka huu ulikuwa ni
fursa kwa Nigeria baada ya kutajwa kuwa nchi yenye uchumi mkubwa Afrika,
lakini mashambulio ya kundi la wapiganaji wa Boko Haram na wasiwasi wa
kiusalama yameugubika mkutano huo.
Hisia mbali mbali zimemiminika kufuatia mashambulio yanayoendelea nchini Nigeria.
Aliyekuwa katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Kofi
Annan, ametoa wito wa hatua kuchukuliwa dhidi ya mashambulio hayo, na
ameishutumu serikali ya Nigeria na mataifa ya Afrika kwa kutochukua
hatua haraka kufuatia utekaji nyara wa wasichana wa shule takriban 200
nchini humo.
Annan ameyaomba mataifa hayo kutumia walichonacho kusaidia kuwaokoa wasichana hao.
Alisema, 'Nadhani Afrika ingekuja pamoja na
kulaani kwa harama kitendo hicho na serikali ya Nigeria nayo
ingewafariji ummma kwa kueleza kwa uwazi juhudi wanazofanya kuwatafuta
na kuwaokoa wsichana hao'.
Msichana wa Pakistani aliyeponea kupigwa risasi
na wapiganaji wa kundi la Taliban, Malala Yousafzai, amesema,
'Wanayofanya ni kinyume kabisa na dini -nawashauri waisome na kuifuata
koran - koran inatoa ujumbe wa amani, utu na uadilifu. Kilichofanyika
kweli kinanihuzunisha'.
Malala ameeleza kwamba dunia haipaswi kunyamaza kuhusu utekaji wa wasichana hao takriban 200 Nigeria.
0 comments:
Chapisha Maoni