Wakati Bunge la Bajeti 2014/15 likiendelea mjini Dodoma na hivi
karibuni viongozi wa dini kutoa ufafanuzi wa kuonekana kwa mwezi
mwekundu na kueleza kwamba unaashiria mwisho wa dunia, mtabiri maarufu
Bongo, Alhaji Maalim Hassan Yahya Hussein amefunguka kwamba hiyo ni
ishara kuwa, wabunge wengi watapoteza nyadhifa zao na viongozi wengi
watakufa.
Akizungumza chanzo chetu cha habari, Maalim Hassan alisema
kuonekana kwa mwezi mwekundu (blood moon) Aprili 15, mwaka huu ni ishara
kwamba viongozi wengi, wakiwemo wa dini na serikali watakufa ghafla na
wengine hasa wabunge watapoteza nyadhifa katika majimbo yao ya uchaguzi
kutokana na sababu mbalimbali.
Mwezi mwekundu ulioonekana ni dalili kwamba kutakuwa na habari nyingi za matatizo, njaa itakuwa kubwa, mashaka, uongo, viongozi kupingana huku wengine wakiondolewa madarakani kama wabunge au kufa ghafla.
Kutatokea mizozo mingi kwa nchi ya Tanzania na nchi za jirani
alisema Maalim Hussein.
Hata hivyo, mtabiri huyo aliwataka watu kuwa na tahadhari kwani Mungu anazungumza nao kwa ishara hizo zinazoonekana na mwezi utapatwa kwa mara ya pili na kuwa mwekundu Oktoba 23, mwaka huu, Jumanne ambayo kinyota ni siku ya mashaka.

0 comments:
Chapisha Maoni