Mwanamume mmoja mjini Hail, nchini Saudi Aarabia
amejitolea na kuweka Jokofu nje ya nyumba yake na kutoa wito kwa
majirani kulijaza na vyakula ili kuwasaidia maskini.
Gazeti la Gulf News linaripoti kuwa, mwanamume
huyo ambaye hakutaka kujulikana aliwaambia majirani wake kuwa jambo hili
litawaondolea maskini aibu ya kuomba chakula.
Watoto wakitia chakula ndani ya majokofu Saudi Arabia |
Habari hizi zilichipuza baada ya
mhubiri mmoja maarufu wa Kiislamu kusifu hatua hio kwenye mtandao wa
twitter. Sheikh Mohamad al-Arefe aliandika kuwa
nimekuwa nikisema watu wa Hail ni wakarimu.
Mwanamume mmoja ameweka jokofu nje ya nyumba
yake ili kuweka mabaki ya chakula: njia ya kuonyesha upendo na kutoa
msaada kwa maskini . Oh, jinsi ninavyoipenda Hail.’ Kauli hiii ya sheikh
Mohamad ilisambazwa zaidi ya mara 5000, kwa mujibu wa mtandao wa habari
wa Akhbar.
Watumiaji wa mitandao ya kijamii wanatoa wito
kwa misikiti na nyumba zingine kuweka nje majokofu kama hatua ya
kuonyesha ukarimu kwa jamii.
Mtu mwingine naye akiongeza sauti yake, amesema kuwa watu wapaswa kuweka chakula ambacho kimepikwa na si mabaki tu.
Aliongeza kusema kuwa ni jambo la kulisha sio
mwili tu bali hata nafsi kupitia vitendo vikuu vya upendo na msaada kwa
maskini hasa kwa muda unaoelekea mwezi mtukufu wa Ramadhan, utakaoanza
rasmi mwishoni mwa mwezi Juni.
0 comments:
Chapisha Maoni