Katika siku za mwanzo tu uhusiano wao, Martha alimpa
utambulisho boyfriend wake Jacob:
Sweetheart, huyu ni rafiki yangu anaitwa Roy, ni mshkaji wangu wa karibu, mimi na yeye ni kama kaka na dada, siri yangu yake, yake yangu. Baadaye ukiniona naye usije kunionea wivu.
Jacob aliitikia kisha maisha yakaendelea. Penzi likakua,
Jacob alimvalisha Martha pete ya uchumba baada ya utambulisho kwa
wazazi kufanyika na kukubalika. Taratibu za ndoa zikashika kasi lakini
kuelekea kuoana, kuna jambo la kushangaza likajionesha.
Siku moja asubuhi, Jacob alifika nyumbani kwa Martha kwa ajili ya kumpelekea matumizi. Alikuta mlango wa sebuleni upo wazi, akaingia na kupitiliza kabisa chumbani. Akastaajabu kumkuta Roy amelala, amejiachia kitandani.
Jacob akasalimia:
Kaka mambo vipi?
Roy akajibu:
Safi kabisa bro.
Namna Roy alivyojibu, alionesha kujiamini kupita kiasi. Mara,
Martha naye akatokea choo cha chumbani akiwa amejifunga kanga moja tu!
Waooo baby umenisapraiz leo asubuhiasubuhi,
Martha alisema.
Jacob akamtoa Martha sebuleni ili wazungumze. Ile wanaketi tu, Martha akalianzisha:
Jacob akamtoa Martha sebuleni ili wazungumze. Ile wanaketi tu, Martha akalianzisha:
Baby usishangae kumkuta Roy hapa, aligombana na mkewe, kwa hiyo ikabidi aje alale hapa.
Kwa nini aje alale hapa tena kitandani kwako kabisa?
Jacob aliuliza.
Ndiyo sweetheart, si unajua Roy anavyonipenda na kunizoea mimi dada yake? Ikabidi aje alale hapa, vinginevyo labda angekwenda kulala hotelini, sasa gharama za nini?
Martha alijibu kwa mtindo wa kuhoji.
Ukaingia chooni kuoga, ukatoka na kanga moja mbele ya Roy, eti kaka yako. Unawezaje kunishawishi nikuamini kuwa wewe na yeye siyo wapenzi?
Jacob
aliuliza.
Martha alijitetea, Jacob akamwambia amemwelewa. Alimkabidhi fedha za matumizi kisha akaaga kuondoka. Martha alimsindikiza, akahakikisha Jacob anaingia kwenye gari na kuanza kuondoka ndipo naye akaingia ndani.
Jacob hakufika mbali, alipoangalia kwenye vioo (side mirrors) na kumuona Martha anarudi ndani, aligeuza gari. Alipofika alipaki na kuanza kutembea kwa kunyata. Mlango wa sebuleni alikuta upo wazi, akapitiliza mpaka mlango wa chumbani.
Pale kwenye mlango wa chumbani, akasikia sauti ya Roy ikiuliza:

Vipi jamaa yako ameondoka?
Martha akajibu:
Bwege yule ameshaondoka, ila kaniuliza maswali magumu? Inaonekana ameshaanza kutushtukia.
Jacob
aliposukuma mlango, aliwakuta Martha na Roy wamelaliana. Walipomwona
walishtuka sana, mwenyewe akawaambia:
Endeleeni na starehe zenu, mimi bwege nilikuwa napita tu!
Baada ya hapo akaondoka zake.
Kuanzia siku hiyo, Jacob alipokea SMS mfululizo kutoka kwa Martha na Roy wakimwomba msamaha kwa waliyomtendea lakini hakujibu hata moja. Walipiga simu lakini hakupokea. Upande wa pili, Martha alimtupia lawama Roy:

Ona umeniharibia ndoa, nitafanya nini mimi na wewe una mke wako?
Baada
ya wiki tatu, Jacob aliwaita Roy na Martha nyumbani kwake ili waende
wakazungumze na kuyamaliza. Walienda haraka sana. Walipofika sebuleni,
Jacob aliwaambia waende mpaka chumbani. Haikuwa shida, Martha anakijua
chumba, kwa hiyo wakaingia.
Mbona ilikuwa sinema? Jacob alikuwa amelala akiwa amemkumbatia mwanamke mrembo anayeitwa Rosemina. Huyo Rosemina ni mke wa Roy. Palepale Roy na Martha waliteleza na kujikuta wamekaa chini kwa mshtuko. Picha ilikuwa wazi kuwa Jacob na Rosemina ni wapenzi, maana hata pale kitandani hawakuwa na nguo iliyowasitiri.
Jacob akafunguka:

Nyie si mlisema mimi ni bwege, sasa nimeamua kuwaonesha ubwege wangu, kuanzia sasa ninyi nendeni mkaoane, mimi nitamuoa Rosemina wangu hapa. Nimempata kwa urahisi kwa sababu naye alikuwa ameshachoshwa na tibia zenu, mnajifanya kaka na dada kumbe mahasidi wakubwa. Na mimi huyu ni dada yangu na hapa namfundisha ‘kitchen party’ ya kitandani.
0 comments:
Chapisha Maoni