Jumapili, Aprili 20, 2014

RAIS KIKWETE AWAKEMEA WANAO WADHIHAKI MWL. NYERERE NA MZEE KARUME AKIWEPO TUNDU LISSU KATIKA VIDEO HII

Msomaji wangu katika mtandao huu wa habari na burudani, najua unakumbuka sana juu ya taarifa niliyowahi kukupatia juu ya mbune wa Singida kaskazini na mwanasheria wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo 'CHADEMA' ama CDM kama ilivyofupishwa zaidi na wapenzi wa chama hicho, mh Tundu Lissu kuwakashifu waasisi wa taifa hili, Mwl. Julius Kambarage Nyerere na mzee Karume kwa kuwaita waongo kwa maana kuwa walikuwa wababaishaji tu!

Nanukuu hapa kauli ya Tundu Lissu aliyoiongea akiwa bungeni Dodoma katika Bunge maalumu la katiba na kama alivyoandika pia kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, Facebook;


Nyerere alikuwa mwongo-mwongo...wamezoea vya haramu, vya halali hawaviwezi,
Sasa baada ya hili mheshimiwa rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho kikwete ameliongelea jambo hilo alilolizungumza Tundu Lissu katika video hii..

0 comments:

Chapisha Maoni