WAZIRI Kivuli wa Mambo ya Ndani, Vincent Nyerere ameibuka na kutoa kauli
ya kutaka Video Queen Agnes Gerald ‘Masogange’ akamatwe na kuswekwa
ndani akidai kitendo cha kuachiwa huru Afrika Kusini kwa kesi ya madawa
ya kulevya si sahihi kwa Bongo.
Akizungumza na Kipindi cha Dakika 45 kilichorushwa hewani Jumatatu
usiku na Runinga ya ITV, Nyerere alisema baada ya uchunguzi kufanyika
ilibainika kuwa yale madawa kwa nchini Afrika Kusini si ya kulevya
lakini kwa Tanzania ni ya kulevya.
Alisema kutokana na kubainika kwamba yalitokea nchini, baadhi ya
wafanyakazi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar
walitimuliwa kazi, akasema basi ilikuwa lazima Masogange baada ya kutua
Bongo akamatwe.
“Mimi nimeshangaa sana jamani, ilikuwaje watu watimuliwe kazini pale
uwanja wa ndege kwa kuwatuhumu kuruhusu madawa ya kulevya kupita, kwa
nini walimuachia huru yule binti (Masogange), basi waliofukuzwa nao
warudishwe kazini,” alisema Nyerere.
Paparazi wetu, juzi alifanya jitihada za kuzungumza na Waziri wa
Uchukuzi, Mheshimiwa Harrison Mwakyembe lakini simu yake ilikuwa ikiita
tu.
Kwa upande wake, Kamanda wa Kikosi Maalum cha Kuzuia na Kupambana na
Madawa ya Kulevya Tanzania, Afande Godfrey Nzowa alipopigiwa simu
alisema kule Afrika Kusini Masogange alipatikana na hatia na kuhumumiwa,
kwa hiyo hakuna sheria ya kumkamata tena hapa nchini.
“Kule alihukumiwa kwenda jela au kulipa faini, ina maana alipatikana
na hatia, akalipa faini na kuachiwa, sasa kwa nini tumkamate huku?”
alihoji Nzowa.
Simu ya Masogenge juzi ilikuwa ikiita mara kadhaa bila kupokelewa.
Simu ya Masogenge juzi ilikuwa ikiita mara kadhaa bila kupokelewa.
Julai 5, mwaka jana, Masogange na Melisa Edward walikamatwa Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo jijini Johannesburg na madawa ya
kulevya aina ya crystal methamphetamine yenye thamani ya shilingi
bilioni 6.8.
Kesi yao iliendeshwa na Mahakama Kuu ya Gauteng iliyopo Kempton Park
nchini humo ambapo Masogange alikutwa na hatia na kuhukumiwa kwenda jela
miezi 32 au faini ya randi 30,000 (shilingi milioni 4.8). Masogange
alilipa huku mwenzake, Melisa akiachiwa huru baada ya kuonekana hakuwa
na hatia.
0 comments:
Chapisha Maoni