Baadhi ya kampuni na wamiliki wa viwanda mkoani Tanga,
wameingiwa na hofu ya kupungua kwa kasi ya uzalishaji wa bidhaa za
viwandani, kufuatia kutokuwepo umeme wa uhakika na ukataji holela wa
huduma hiyo.
Hayo yalielezwa jana katika kongamano la wadau wa
watumiaji wa umeme Kanda ya Kaskazini, lililofanyika mjini hapa na
kuelezwa kuwa, ili kuwavuta wawekezaji wa ndani na nje, Serikali
ilipatie ufumbuzi tatizo la umeme.
Walisema kutokuwepo kwa umeme wa uhakika ni chanzo
cha uzalishaji mdogo wa bidhaa viwandani, jambo linalochangia kupunguza
wafanyakazi wa viwandani.
Ilielezwa Serikali imekuwa ikikosa mapato kutokana na wawekezaji kushindwa kuzalisha bidhaa.
0 comments:
Chapisha Maoni