Jumatano, Machi 12, 2014

DIAMOND KUHOJIWA NA WANAUSALAMA BAADA YA ALI KIBA KUTISHIWA KIFO

SAKATA la staa wa Bongo Fleva, Ally Saleh ‘Ali Kiba’ kunusurika kuuawa na watu wasiojulikana kwa kutumia bastola limechukua sura mpya, safari hii, Nasibu Abdul ‘Diamond’ amefunguka kuwa amejiandaa kuhojiwa na polisi.
Kwa mujibu wa chanzo chetu katika jeshi hilo jijini Dar, Diamond ambaye amekuwa akitajwa sana katika sakata hilo kupitia mitandao ya kijamii ataitwa kuhojiwa.
“Unajua ile kesi ipo hapa Central, awali ilitokea Polisi Msimbazi, sasa mpelelezi wake amekuwa akifikiria kumwita Diamond ili amhoji maana anatajwa sana,” kilisema chanzo hicho.
Hivi karibuni, Ali Kiba alivamiwa usiku na watu zaidi ya watano nyumbani kwao, Kariakoo jijini Dar ambapo waliruka ukuta na kuingia ndani huku kila mmoja akiwa na bastola.
Ilidaiwa kuwa, mmoja kati ya watu hao ambao ilisemekana walitumwa kumuua msanii huyo, aliibua mzozo wa makusudi kwa wenzake ili kumpa mwanya Kiba kutoroka kwa vile hakufurahishwa na kitendo hicho.
 Habari zinasema walipoingia ndani huku kelele za mbwa zikasaidia kumshtua staa huyo, ule mzozo ulioanzishwa na wavamizi hao ulimsaidia Kiba kutoroka ingawa walimkosakosa risasi.
Ikasemekana baada ya msanii huyo kukimbia, jamaa ambaye alimkingia kifua alimpigia simu na kumfungukia watu waliohusika huku ikidaiwa kuwa baadhi yao ni mastaa wenzake.
“Alinitajia tu majina lakini nilishindwa kuthibitisha moja kwa moja hivyo nikayafikisha Kituo Kikuu cha  Polisi (Central) kwa ajili ya uchunguzi,” alisema Ali Kiba huku akikataa kutaja hata jina moja.
Hata hivyo, mengine yaliibuka hasa kwenye mitandao ya kijamii kuwa, miongoni mwa wasanii waliohusika katika tukio hilo eti ni na Diamond.
Amani lilimsaka afande mmoja ambaye anajua mwenendo wa kesi hiyo ambaye alikiri kesi hiyo kuwepo Central lakini alisema mambo yote ni siri ya kazi.
“Nani atahojiwa, nani hatahojiwa ni siri ya kazi yetu,” alisema.
Juzi, paparazi wetu walimtafuta staa huyo wa Wimbo wa Number One ili kusikia anazungumziaje manenomaneno hayo ya kwenye mitandao na vinywa vya watu.
“Nimeshasikia nikitajwa katika hilo, kimsingi ni madai mazito lakini mimi nipo tayari kuhojiwa ili sheria ichukue mkondo wake kwani najua si kweli na sijui lolote,” alisema Diamond.
Akandelea: “Mimi na Kiba kuna ugomvi gani hadi nifikie hatua hiyo. Kwanza sina moyo wala uwezo wa kufanya hivyo.”

0 comments:

Chapisha Maoni