Watu wasiopungua 200 wameuawa na makumi ya wengine
kujeruhiwa baada ya watu wasiojulikana kushambulia vijiji vitatu
katikati mwa Nigeria.
Taarifa zinasema kuwa, karibu watu 200 wameuawa baada ya watu
wanaobeba silaha kushambulia na kuchoma moto vijiji vitatu vya Ugwar
Sankwai, Ugwar Gata na Chenshyi vilivyoko katika jimbo la Kaduna.
Taarifa zinasema kuwa, watu waliotekeleza shambulio hilo ni kutoka
kabila la Fulani. Afisa mwandamizi wa polisi katika jimbo la Kaduna
amethibitisha k
utokea kwa shambulio hilo. Shambulio hilo limetokea
katika eneo ambalo mara kwa mara limekuwa likigubikwa na mapigano ya
kidini na ugomvi wa ardhi. Shambulio hilo la jana limetokea katika hali
ambayo, siku ya Jumamosi kwa akali watu 212 waliuawa katika mapigano
yaliyotokea kati ya jeshi la Nigeria na wanamgambo wa kundi la Boko
Haram katika eneo la Maiduguri lililoko katika jimbo la Borno. Taarifa
zinasema kuwa, wanamgambo 207 wa Boko Haram na wanajeshi watano wa
serikali ya Nigeria waliuawa kwenye mapigano hayo.
0 comments:
Chapisha Maoni