Umoja wa Katiba ya Watanzania (Ukawa), walitangaza mapema jana
kwamba wangepinga ratiba nzima kuendelea hadi madai yao ya kumtaka Rais
Jakaya Kikwete afungue Bunge kwanza kabla ya rasimu kuwasilishwa
yasikilizwe.
Madai ya Ukawa
Viongozi wa Ukawa waliitisha mkutano wa wanahabari
na kutangaza kususia kuendelea na ratiba wakipinga uvunjwaji wa kanuni
unaodaiwa kufanywa na Sitta.
Katika uamuzi huo uliofikiwa jana mchana, mmoja wa
viongozi wa Ukawa, Profesa Ibrahimu Lipumba alisema: “Kwa sababu za
ukiukwaji wa kanuni, tunapenda kueleza kwamba hatupo tayari kuunga
mkono, tutapinga kwa kadri ya uwezo wetu, mambo makubwa manne kufanyika
bungeni.”
Alisema mambo ambayo wanapinga ni uwasilishaji wa
Rasimu ya Katiba uliopangwa kufanyika jana kabla ya ufunguzi wa Bunge
maalumu unaotarajiwa kufanywa na Rais Jakaya Kikwete.
Profesa Lipumba pia alisema wangepinga kufanyika
kwa semina ambayo ilipangwa kuongozwa na wataalamu wa ndani au nje ya
nchi leo kuhusu uzoefu katika masuala ya Bunge la Katiba.
“Pia tutapinga hotuba ya Rais endapo itatolewa
baada ya uwasilishaji wa Rasimu ya Katiba na pia jambo jingine lolote
linalokiuka Kanuni za Bunge Maalumu,” alisema Profesa Lipumba
aliyeambatana na wajumbe wenzake, James Mbatia na Tundu Lissu.
Kanuni zinazolalamikiwa
Profesa Lipumba alisema mara baada ya kuchaguliwa,
Sitta amevunja Kanuni ya 7 (1) (g) na (h) ambazo zimeweka mpangilio wa
shughuli zote za Bunge Maalumu.
“Hotuba ya ufunguzi ambayo itatolewa na Rais,
ilielezwa wazi kwenye kanuni kuwa itatangulia na kufuatiwa na
uwasilishaji wa Rasimu ya Katiba. Hivyo kwa kutangaza kuanza kuwasilisha
rasimu ni kuvunja kanuni,” alisema.
0 comments:
Chapisha Maoni