Kampuni nyingi za simu na za madini nchini zinadaiwa kuwanyonya
wafanyakazi wao na kusababisha serikali kuamua kuingilia kati kwa
kusimamia moja kwa moja usajili mpya wa mawakala wa ajira.
Kampuni hizo zinatuhumiwa kutumia mawakala kupata
wafanyakazi kinyume na utaratibu wa kisheria, kuingia mikataba na
mawakala hao, kuwalipa mishahara kisha mawakala kulipa wafanyakazi,
ikiwa ni ujanja wa kuepuka kuwajibika moja kwa moja kwa wafanyakazi hao.
Kwa mujibu wa sheria, mawakala hao ambao awali
walikuwa wakisajiliwa na Msajili wa Kampuni (Brela) na Wakala wa Ajira
nchini (Taesa), walitakiwa kuwa kiunganishi kati ya waajiri na watafuta
kazi kwa kulipwa kamisheni, lakini wamekuwa wakikodisha wafanyakazi kwa
kampuni hizo kinyume cha sheria.
Msemaji wa Wizara ya Kazi na Ajira, Ridhiwan Wema
alisema jana kuwa Wizara iliamua kuingilia kati suala hilo na kusimamia
moja kwa moja usajili mpya wa mawakala hao kwa kuwa ilibaini ukiukwaji
mkubwa wa sheria, ikiwamo kuwanyima haki zao za matibabu, pensheni na
kuikosesha Serikali mapato yanayotokana na mishahara yao.
Kampuni hizo ndizo zinazotengeneza faida kubwa na
zinazojiendesha kwa gharama za juu, huku zikipata ahueni ya kodi kutoka
serikalini.
Mawakala 56 binafsi wa ajira wameshajiorodhesha na wizara imeongeza miezi miwili zaidi kwa ajili ya usajili huo.
0 comments:
Chapisha Maoni