Watafiti nchini Uingereza wamegundua kuwepo Saratani
katika mifupa ya kijana mmoja aliyeishi nchini Misri miaka elfu tatu
iliyopita.
Hii ni miaka elfu mbili kabla ya kisa cha kwanza cha ugonjwa huo kuthibitishwa.
Mtafiti Michaela Binder, aligundua kuwa mifupa hiyo, ilikuwa na mashimo, na kugundua kuwepo aina ya Saratani katika mifupa hiyo.
Ugunduzi huu unaonyesha kuwa Saratani sio
ugonjwa wa kisasa tu na hivyo wanasayansi watapata kuchunguza ambavyo
ugonjwa huu ulianza miaka zaidi ya elfu moja iliyopita.
0 comments:
Chapisha Maoni