Serikali ya mpito ya Misri imeimarisha usalama kufuatia
shambulizi lililofanywa kwenye kituo cha upekuzi cha kijeshi huko Cairo
mji mkuu wa nchi hiyo.
Watu waliokuwa na silaha jana walikishambulia kituo kimoja cha
upekuzi mjini Cairo na kuwauwa wanajeshi sita. Serikali ya mpito ya
Misri kwa upande wake imeeleza kuwa imeamua kupambana na yeyote
atakayejaribu kuwashambulia raia na maeneo ya serikali na kwamba
mashambulizi dhidi ya jeshi yatashughulikiwa na mahakama za kijeshi.
Serikali hiyo ya mpito ya Misri imeongeza kuwa imeamua kuimarisha
hali ya usalama nchini humo ili kuzuia wimbi la mashambulizi
yaliyopelekea kuuliwa wanajeshi wasiopungua 300 tangu kuanza
mashambulizi hayo baada ya kupinduliwa na jeshi mwezi Julai mwaka jana,
Mohamed Morsi Rais wa kwanza kuwahi kuchaguliwa kidemokrasia huko Misri.
Jeshi la Misri limeinyoshea kidole cha tuhuma harakati ya Ikhwanul
Muslimin na wafuasi wa Mohamed Morsi, hata hivyo ushahidi mdogo
umetolewa kuweza kuyapa nguvu madai hayo. Ikhwanul Muslimin pia
imekanusha kuhusika na mashambulizi hayo.
0 comments:
Chapisha Maoni