Meneja wa zamani wa Manchester United,Sir Alex Ferguson anaamini
David Moyes atakuwa na mafanikio makubwa klabuni hapo na angepaswa
kupewa muda zaidi ili kuimarisha kikosi hicho cha Old Trafford.
Moyes amekuwa akijadiliwa sana kutokana na kazi aliyoifanya Man United tangu achukue nafasi ya Ferguson majira ya joto.
Man United ambao hawakucheza wikiendi iliyopita wakiwa nafasi ya saba
kwenye msimamo wa ligi kuu ya Uingereza,wapo nyuma ya vinara Chelsea
kwa pointi 18 na wanahali mbaya katika michuano ya ligi ya mabingwa
barani Ulaya mara baada ya kufungwa goli 2-0 na Olympiakos pale
Athens,Ugiriki.
Kukosa kwenye michuano ya Ulaya kwa Man United ni kitu kitakachosikitisha
sana kwa klabu hiyo ambayo alishatolewa kwenye kombe la FA na Swansea
na kombe la Capital One na Sunderland ambayo ilifungwa fainali na Man
City siku ya Jumapili huku mashetani wekundu wakitolewa mara zote hizo
ndani ya dimba la Old Trafford.
Pia mabingwa hao watetezi wapo nyuma ya timu inayoshika nafasi ya
nne,Manchester City kwa pointi 12 na wanahaha kutafuta tiketi ya
kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya huku matumaini ya
kutetea taji yakiwa yamefifia kabisa.
Ferguson ambaye alikaanza kuinoa Man United mwaka 1986 nakusubiri
mpaka mwaka 1990 kabla ya kupata taji lake la kwanza anahisi kuwa Moyes
anaweza kupata mafanikio na anadhani anahitaji muda zaidi ili kuweza
kuboresha timu na kuonyesha ubora wake.
Raia huyo ya Scotland alisisitiza kuwa,”Man United itakuwa sawa.Ni
mapema sana na kumekuwa na mabadiliko makubwa.Moyes anahitaji muda.”
Ferguson aliongeza kuwa,”Nilikuwa pale kwa miaka 27,hivyo kuwa na meneja mpya,inachukua muda lakini watakuwa vizuri tu.






0 comments:
Chapisha Maoni