Jumanne, Machi 04, 2014

RAIS PUTIN ATOA TAMKO KWA MAJESHI YA URUSI

Rais Vladimir Putin wa Urusi amewaamuru wanajeshi wake waliohusika katika luteka za kijeshi ambazo baadhi zikifanyika karibu na Ukraine warudi kwenye kambi zao. Hayo ni kwa mujibu wa msemaji wake Dmitri Peskov.
Luteka hizo zilizokuwa na lengo la kuonyesha utayarifu wa majeshi ya Urusi, ni jambo lililozitia wasiwasi serikali za nchi za magharibi baada ya Urusi kutuma mamiaya wanajeshi katika eneo lina Ukraine la Crimea ambako wakaazi wake
wengi ni wenye asili ya urusi, ikiwa ni baada sya kuangushwa rais wa zamani Viktor yanukovich na wapinzani wanaoelemea upande wa magharibi.
“Luteka hizo zilizoanza wiki iliopita zitamalizika kama ilivyo pangwa,"hivyo ndivyo alivyoeleza msemaji huyo
Haikuweza kufahamika wazi ikiwa hatua hiyo ya rais Putin ni jaribio la kuitekea baadhi ya wito wan chi za magharibi kuutuliza mzozo huo ambao umeupa mtihani mkubwa mustakbali wa Ukraine .

0 comments:

Chapisha Maoni