Jamaa za abiria wa China waliokuwa kwenye ndege ya Malaysia
iliyopotea,wametisha kususia chakula ikiwa maafisa wa utawala wa Malaysia
watakosa kutoa taarifa kamili kuhusu ndege hiyo siku 11 zilizopita.
Jamaa hao wameelezea kukerwa mno
baada ya mkutano na maafisa wa shirika la ndege hiyo mjini Beijing.
Maafisa wa Malaysia nao wanasema
kuwa wanafanya kila wawezalo katika kuisaka ndege hiyo.
Ndege hiyo MH370 ilitoweka tarehe
nane mwezi Machi ikiwa imewabeba watu 239.
Nchi 25 zinahusika na juhudi za
kuisaka ndege hiyo huku China ikianza kuitafuta katika ardhi yake.
Watu 153 raia wa China walikuwa
kwenye ndege hiyo iliyokuwa inatoka Kuala Lumpur kuelekea Beijing.
Vyombo vya habari nchini China
vimekuwa vikikosoa juhudi za Malaysia katika kuitafuta ndege hiyo.
Baadhi ya jamaa za wachina wanasema
kuwa wanaamnini serikali ya Malaysia imebana taarifa kuhusu ndege hiyo na
wanataka maelezo zaidi kuihusu.
Baada ya kukutana na maafisa wa
shirika la ndege siku ya Jumanne, familia za waliokuwa kwenye ndege hiyo
walitishia kususia chakula
"Tunachokitaka ni ukweli,''
alisema mwanamke mmoja.
Wakati huohuo, nchi jirani ya
Malaysia, Thailand imesema kuwa jeshi lake limetambua kile linachosema ni Data
za mtambo wa Rader ambazo huenda zilitoka kwenye ndege hiyo.
Inasema kuwa ndege hiyo ilikuwa
inaelekea Magharibi baada ya kupoteza mwelekeo. Hii inathibitisha madai ya hapo
ya awali ya jeshi la Malaysia.
0 comments:
Chapisha Maoni