STAA wa sinema za Kibongo, Wastara Juma ametoboa kuwa, kuna wanaume
kibao walimchumbia kwa nyakati tofauti, lakini wakabadilisha uamuzi huo
na hivyo kumfanya aendelee kubaki mpweke.
Akizungumza na Risasi Mchanganyiko, wikiendi iliyopita jijini Dar es
Salaam, Wastara alisema, wanaume hao wanafikia uamuzi huo kutokana na
magazeti na mitandao mbalimbali kuripoti mara kwa mara kuhusu uhusiano
wake na Mtangazaji wa Channel Ten, Bond Binslum, habari ambazo
anazikanusha.
Wastara alisema, tangu kifo cha
mume wake, Juma Kilowoko ‘Sajuki’, magazeti yamekuwa yakimwandama kwa
habari za skendo badala ya kuangalia mambo ya msingi na hivyo kumkosesha
mume mwema.
“Maisha yangu ni kama yanaendeshwa na magazeti, kila siku utakuta habari zangu kwenye magazeti tena siyo nzuri, sasa zinanisababishia matatizo.
“Maisha yangu ni kama yanaendeshwa na magazeti, kila siku utakuta habari zangu kwenye magazeti tena siyo nzuri, sasa zinanisababishia matatizo.
Angalia sasa, kuna watu walijitokeza na kuonyesha nia ya kunioa,
lakini wakija kuona habari kwenye magazeti wanabadilisha mawazo.
“Kwa kweli nawashukuru sana nyie (Global) huwa hamuandiki habari bila kuniuliza kwenye simu, lakini wapo wengine sijui wanatoa wapi maneno, wanayaweka kwenye gazeti hivyo hivyo. Yaani tangu nimepata misukosuko, sijatulia kabisa, kila siku ni mikasa baada ya visa,” alisema.
“Watu wanaandika mimi nina uhusiano na Bond, tangu lini? Hata wakiniuliza nikikataa, bado wanaendelea kuandika kuwa Bond ni mpenzi wangu, si jambo la kweli. Sikia... kuna mwanaume mstaarabu sana, tena Muislam safi, alijitokeza nyumbani kistaarabu, akaniposa.
“Mambo yakaenda vizuri, lakini baadaye kidogo akaja kusoma kwenye magazeti eti mimi na Bond tunapika na kupakua, akabadilisha mawazo. Ilikuwa kazi ngumu kumuelewesha kuwa siyo kweli, hakuniamini kabisa.”

“Mwingine tulifikia mahali pazuri kabisa, hadi mahari alishatoa,
baadaye akaona kwenye mitandao kuwa nimeonekana kwenye magazeti nikiwa
na Bond, akahairisha kila kitu na akataka arudishiwe mahari yake -
akapewa.
Hebu angalia ni mambo gani hayo?
“Huko ni kuharibiana. Naishi maisha ya huzuni kila siku, kwanini wasiandike mambo ya msingi ya kunisaidia badala ya kuzusha mambo kama wanavyofanya sasa?”
“Huko ni kuharibiana. Naishi maisha ya huzuni kila siku, kwanini wasiandike mambo ya msingi ya kunisaidia badala ya kuzusha mambo kama wanavyofanya sasa?”
“Mimi ni mwanamke,
nimekamilika. Siwezi kuishi peke yangu siku zote, kwa hiyo kuwa na
mwanaume siyo kosa, ila sasa muda haujafika. Nikiwa na mtu wangu, kwa
nini nisiwe mkweli? Habari za mimi kuwa na Bond zinazushwa tu, watu
waachane na hayo mambo wafanye mengine ya muhimu.
“Kwa sasa niachwe nipumzike, najua ipo siku atatokea mwanaume wa
ukweli, tutakamilisha taratibu zote, atanioa. Ikifika hatua hiyo,
sitakuwa na sababu ya kuficha. Watu wanipe muda kwanza.”
Risasi Mchanganyiko liliwasiliana na mmoja wa mashosti wa karibu na
Wastara na kuzungumza naye kuhusiana na malalamiko ya Wastara ambapo
alisema inawezekana shoga yake akawa na hoja lakini bado ishu hiyo ipo
mikononi mwake.
Kwa sharti la kutotajwa gazetini, shosti huyo alisema: “Lakini rafiki
yangu naye kayataka mwenyewe. Kama hatoki na huyo Bond, sasa mapicha
aliyokuwa akiyaweka kwenye mitandao ya kijamii akiwa naye karibu ya
nini? Maana chanzo cha yote ni hizo picha.
“Namshauri tu atulie, afanye mambo yake kimyakimya, kuweka picha
kwenye mitandao ni hatari... yeye mwenyewe anaamua kuyaendesha maisha
yake kupitia vyombo vya habari.
0 comments:
Chapisha Maoni