Wanajeshi wa Chad waliotumwa kulinda usalama wa raia
katika Jamhuri ya Afrika ya Kati wamewafyatulia risasi raia huko Bangui
mji mkuu wa nchi hiyo na kusababisha vifo vya raia wanane.
Bado haijafahamika nini kilisabababisha ufyatuaji risasi huo uliopelekea kujeruhiwa pia watu wengine kadhaa.
Baadhi ya ripoti zinasema kuwa idadi ya wahanga huwenda ikaongezeka.
Matukio yamekuwa yakijiri kati ya wanamgambo wa Kikristo wa Anti-Balaka
na wanajeshi wa Chad huko Bangui.
Wanajeshi wa Chad ni sehemu ya kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa
Afrika kilichotumwa huko Jamhuri ya Afrika ya Kati kusaidia kukomesha
machafuko yanayoendelea sasa nchini humo kati ya jamii ya Waislamu na
Wakristo yaliyoibuka mwaka uliopita.
Ikumbukwe kuwa Umoja wa Afrika umelitangaza kundi hilo la Kikristo kuwa ni la kigaidi.
0 comments:
Chapisha Maoni