Wahamiaji wenye asili ya Afrika waliokimbilia katika ardhi za
Palestina zilizopachikwa jina la Israel wamefanya maandamano
kulalamikia ubaguzi wanaofanyiwa na viongozi wa utawala wa Kizayuni.
Wanaharakati wa haki za binadamu nao wameshiriki kwenye maandamano
hayo kuwaunga mkono wakimbizi hao wa Kiafrika na kulaani siasa za
kibaguzi za Israel dhidi ya wageni.
Itakumbukwa kuwa, mwaka jana bunge la Israel lilipitisha sheria
iliyolalamikiwa sana ambayo imewapa ruhusa viongozi wa utawala wa
Kizayuni kuwatia mbaroni wahamiaji wa Kiafrika na kuwaweka korokoroni
kwa muda wa mwaka mzima bila ya kuwafikisha mahakamani.
Sheria hiyo imepitishwa na Wazayuni licha ya kwamba makumi ya maelfu
ya wahajiri wanaofanya kazi huko Israel wanatoka katika nchi zenye
migogoro kama vile Eritrea na Sudan Kusini.
0 comments:
Chapisha Maoni