Uchaguzi wa mabaraza ya miji unafanyika leo nchini Uturuki,
ambako zaidi ya wananchi milioni 50 waliotimiza masharti ya kupiga kura
wanatarajiwa kupiga kura.
Matokeo ya uchaguzi huo hasa katika miji ya Ankara na Istanbul
yatadhihirisha nafasi ya kisiasa ya Waziri Mkuu Recep Tayyip Erdogan na
mustakbali wa chama chake tawala cha AKP.
Chama cha Erdogan kinakabiliwa na ushindani mkubwa kutoka vyama
vingine 6 vikubwa vya Uturuki vinavyoshiriki uchaguzi huo hasa chama cha
upinzani cha CHP. Kwa miezi 10 iliyopita serikali ya Erdogan imekuwa
ikikabiliwa na maandamano ya kupinga serikali, huku Waziri Mkuu huyo na
wafuasi wa chama cha AKP wakikabiliwa na kashfa za ubadhirifu.
0 comments:
Chapisha Maoni