Kuthibitishwa kesi mpya za ugonjwa wa Ebola katika mji mkuu
wa Guinea Conakry kumezidisha wasiwasi wa kusambaa virusi vya ugonjwa
huo hatari nje ya mipaka ya nchi hiyo.
Senegal jana ilifunga mipaka yake na Guinea ili kujaribu kuzuia
kuenea Ebola, huku maafisa wa nchi jirani za Liberia na Sierra Leone
wakifanya uchunguzi juu ya ugonjwa huo.
Watu 70 wamefariki dunia kutokana na ugonjwa huo nchini Guinea na
wengine 111 wameambukizwa. Wizara ya Afya ya Guinea imetangaza kuwa,
katika mji mjuu Conakry watu 8 wameambukiwa Maradhi hayo.
Shirika la Afya Duniani WHO limetangaza kuwa, mlipuko wa Ebola hivi
sasa unahesabiwa kuwa mbaya zaidi tangu mwaka 2007 ambapo watu 187
walipoteza maisha kutokana na ugonja huo katika Jamhuri ya Kidemokrasia
ya Kongo. Dalili za homa ya Ebola ni kuhara na kutapika sambamba na joto
kali mwilini ambalo pia huandamana na uvujaji mkubwa wa damu. Homa ya
Ebola huambukizwa kwa kugusa damu, jasho na kinyesi cha mtu mwenye
virusi hivyo.
0 comments:
Chapisha Maoni