Wajordan wamefanya maandamano kupinga mpango wa usalama
uliopendekezwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani John Kerry kuhusu
Palestina.
Maandamano hayo yaliyofanyika mjini Amman, mji mkuu wa Jordan
yamefanyika kupinga mpango huo wa usalama uliowasilishwa na Kerry kati
ya Wapalestina na utawala haramu wa Kizayuni wa Israel. Waandamanaji hao
wameutaja mpango huo kuwa wenye lengo la kuangamizwa kabisa kadhia
nzima ya Palestina. Aidha waandamanaji hao waliokuwa wameshikilia
bendera za Palestina, walitangaza kuwa utukufu wa Palestina ni utukufu
wa Jordan na kusisitiza juu ya hatari ya utawala huo bandia wa Kizayuni
kwa nchi za eneo zima la Mashariki ya Kati. Wajordan hao waliokuwa
wamejawa na hasira kali, walitoa nara dhidi ya Marekani na kuiunga mkono
Qudsi na msikiti wa al-Qudsi Tukufu. Kwa mujibu wa mpango huo wa
Marekani, karibu vitongoji vyote vya walowezi wa Kiyahudi katika Ukingo
wa Mto Jordan, vitaendelea kuwa vya Wazayuni, huku karibu asilimia 80 ya
maeneo muhimu yenye vitongoji hivyo yakitakiwa kukabidhiwa kwa utawala
huo pandikizi wa Kizayuni.
0 comments:
Chapisha Maoni