Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Mbeya imekiri kuwepo
kwa utitiri wa kodi kwa wafanyabiashara ambazo sasa ni kero kwao na
kwamba sasa inaangalia upya njia sahihi ya kuzikusanya kwa pamoja.
Afisa Elimu kwa Mlipakodi wa TRA wa Kanda ya
Nyanda za Juu Kusini, Kissa Kyejo alitoa kauli hiyo mjini Chunya juzi,
wakati akijibu kero mbalimbali za wafanyabiashara, kwenye semina
iliyoandalia na TRA.
Semina hiyo ilihusu umuhimu kwa mfanyabiashara kulipa kodi kwa kutumia Mfumo wa Mashine za Ki-eletroniki (EFDs).
Kissa alisema wafanyabiashara maeneo mengi wamelalamikia kuwapo kwa utitiri huo na kwamba hata TRA wameliona, na sasa walishapeleka ombi kwao ili ziweze kuunganishwa kwa pamoja.
Kissa alisema wafanyabiashara maeneo mengi wamelalamikia kuwapo kwa utitiri huo na kwamba hata TRA wameliona, na sasa walishapeleka ombi kwao ili ziweze kuunganishwa kwa pamoja.
Awali wafanyabiashara hao walilalamikia kuwapo
aina mbalimbali za kodi ambazo walidai zimekuwa kero kubwa kwao,
ikiwamo usumbufu wanaoupata kutoka kwa maafisa wa Serikali.
Mfanyabiashara wa Chunya Mjini, Ayubu Omari
alisema: “Leo anakuja mtu wa TRA, tunamalizana naye, kesho mtu wa ardhi,
mara wa maji, hujakaa sawa watu wa halmashauri nao wamefika wanataka
ushuru. Sasa huu utitiri wa kodi kwetu tunaona ni usumbufu na kero.’’
Akifungua semina hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Chunya,
Deodatus Kinawiro aliwataka wafanyabiashara hasa wachimbaji wadogo wa
dhahabu kupitia Chama cha Wachimbaji Madini Mkoa wa Mbeya, (Mberema)
kuanza kulipa kodi. Alisema wachimbaji wengi wanapata fedha nyingi,
lakini hawalipi kodi na hivyo kuikosesha serikali mapato.
0 comments:
Chapisha Maoni