Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas imelaani
vikali hatua ya Misri ya kukifunga kivuko cha mpakani cha Rafah
kinachotumiwa kama njia ya kuingilia eneo la Ukanda wa Ghaza.
Fauz Barhum, msemaji wa harakati ya Hamas ameeleza kuwa hatua hiyo ya
serikali ya mpito ya Misri inayoungwa mkono na jeshi ni jinai dhidi ya
ubinadamu. Barhum amesema kuwa sisitizo la maafisa wa Misri la kukifunga
kivuko cha Rafah na kushadidisha mzingiro wa Ghaza, ni jinai dhidi ya
ubinadamu kwa viwango vyote na pia ni jinai dhidi ya raia wa Palestina.
Umoja wa Mataifa pia umelaani hatua ya Misri ya kukifunga kivuko cha
Rafah na kusema kuwa unatiwa wasiwasi na raia wa Palestina wanaohitajia
huduma za matibabu huko Ukanda wa Ghaza. Raia wa Palestina hutumia
kivuko cha Rafah kuingia na kutoka katika Ukanda wa Ghaza ulioko chini
ya mzingiro wa utawala wa Kizayuni wa Israel ili kujidhaminia mahitaji
yao muhimu.
0 comments:
Chapisha Maoni