Mahakama moja ya Cairo Misri imemhukumu kifungo cha miaka
kumi jela polisi mmoja wa nchi hiyo kwa kuhusika mwaka uliopita na vifo
vya wanachama wa harakati ya Ikhwanul Muslimin wanaokaribia 40 waliokuwa
kizuizini.
Vyombo vya mahakama vimeeleza kuwa polisi wengine watatu pia
wamehukumiwa vifungo vya nje. Wizara ya Mambo ya Ndani ya Misri imeeleza
kuwa wafuasi hao wa Ikhwanul Muslimin walifariki dunia katika jaribio
la kuvunjwa jela baada ya kukosa hewa mara baada ya kuvuta gesi ya kutoa
machozi katika tukio la mwezi Agosti mwaka jana.
Hata hivyo duru nyingine zinasema kuwa watu hao waliaga dunia kwa
kukosa hewa ya kutosha wakiwa wamepakiwa nyuma ya gari la polisi wakati
wakipelekwa jela nje ya mji wa Cairo. Takwimu mpya zinaonyesha kuwa
serikali ya mpito ya Misri inayoungwa mkono na jeshi imewafunga jela
karibu watu 16,000 tangu mwezi Julai mwaka jana, wakati alipopinduliwa
Rais halali wa nchi hiyo Muhammad Morsi.
0 comments:
Chapisha Maoni