Mafuriko yaliyosababishwa na mvua kali zilizonyesha huko
Afrika Kusini yameua watu 32 na kupelekea maelfu ya wengine kukosa
makazi.
Andries Nel Naibu Waziri wa Utawala wa Ushirika na Masuala ya
Utamaduni wa Afrika Kusini amesema kuwa mvua kubwa iliyonyesha nchini
humo imeua watu 32 na kupelekea wengine 3000 kuzihama nyumba zao katika
manispaa ya Lephalale kaskazini mwa nchi hiyo.
Amesema watu 25 wamefariki dunia kwa kuzama majini, sita kwa radi na
mmoja kwa kuangukiwa na ukuta. Waziri huyo wa Afrika Kusini amesema kuwa
oparesheni za uokoaji kwa wale wote waliokumbwa na mafuriko zinaendelea
na zoezi la kuwatafuta watu waliopotea tayari limeanza. Afrika Kusini
imekumbwa na mvua nyingi na zisizosita katika kipindi cha wiki mbili
zilizopita huku maeneo yaliyoathiriwa vibaya yakiwa ya upande wa
kaskazini na mashariki mwa nchi hiyo.
0 comments:
Chapisha Maoni