Mwenyekiti
wa Bunge Maalum la Katiba, Samuel Sitta, ametangaza kufuta semina zote
za masuala ya uelewa kuhusu Muungano ambazo zilipaswa kufanyika.
Hata hivyo, semina ya kupata uzoefu kutoka Kenya imebaki hivyo na
inatarajia kufanyika leo na wageni wataalamu kutoka nchi hiyo wataeleza
mchakato na namna walivyokubaliana hadi kufikia kupata katiba yao.
Hayo yalisemwa jana asubuhi na Sitta kabla ya kuanza kwa shughuli za uapishaji kwa wajumbe wa Bunge hilo ambao hawapishwa.
Sitta alitoa ufafanuzi juu ya mambo waliyokubaliana ndani ya kikao kilichofanyika juzi usiku baada ya kukubaliana kwa pande mbili zilizokuwa zikipingana.
Kikao hicho kilifanyika kufuatia vurugu zilizozuka ndani ya bunge kwa baadhi ya wajumbe kupinga Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, kunyimwa muda wa kutosha wa kuwasilisha taarifa yake.
Suala lingine ambalo lilizua utata ni pamoja na kukiukwa kwa kanuni ya 7 (g) na (h) ambavyo vinatoa nafasi kwa Rais kutangulia kuzindua Bunge kabla ya mwenyekiti wa tume kuwasilisha rasimu.
Hata hivyo, jana aji Warioba aliwasilisha Rasimu hiyo.
Awali ilipangwa kuwa wajumbe wa bunge hilo wangepata semina ya kujifunza zaidi kutoka kwa wakongwe juu ya masuala ya Muungano na historia ya nchi mbili za Tanganyika na Zanzibar.
Waliotarajia kutoa semina hiyo ni Ramadhani Omari Mapuri na Wadil Kavishe kutoka Zanzibar wakati kwa upande wa Bara walialikwa Hassan Ngwilizi na Profesa Issa Shivji.
Semina hiyo ilikuwa ikileta utata na ilihojiwa na wajunbe wengi wakisema kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinatumia nafasi hiyo kuzima midomo ya wajumbe kutoa maoni yao kwa uhuru.

0 comments:
Chapisha Maoni