Shirika la kutetea haki za binadamu la Huma Rights Watch limeituhumu serikali ya Ethiopia kwa kuwapeleleza wapinzani wake.
.Kwa mujibu wa shirika hilo, serikali hunasa mawasiliano yao kupitia kwa simu zao za mkononi au kompyuta zao
Shirika hilo limesema kuwa maafisa
wa utawala Ethiopia wamenunua programu na vifaa vya kunasa mawasiliano
kutoka Ulaya na nchini China , katika mpango wake wa kukandamiza
wapinzani.
Raia wa Ethiopia wanaoishi Uingereza na nchini
Marekani pia wameituhumu serikali mjini Addis Ababa kwa kutumia programu
hizo kunasa mawasiliano katika kompyuta zao.
Waziri wa mawasiliano wa Ethiopia amekanusha madai hayo.
Hata hivyo shirika hilo limesema kuwa liliwahoji zaidi ya watu miamoja ikiwemo majasusi wa zamani.
0 comments:
Chapisha Maoni