Familia za abiria wa ndege iliyotoweka ya Malaysia majuma
mawili yaliyopita, wamekabiliana na polisi nje ya ubalozi wa Malaysia
mjini Beijing.
Wakiwa wamejawa na ghadhabu, wamelitaka shirika la ndege ya taifa hilo mjini Kuala Lumpur kueleza kilIchofanyika.
Jamaa hao walibeba mabango yenye maandishi “Save MH370″ jamaa hao
wenye hasira walikabiliana na polisi na kuwalemea hadi kuingia katika
ofisi ya ubalozi huo.
Walifoka wakisema ..”Tunataka ukweli.” hii ni ishara ya hasira na mafadhaiko wanayopitIa jamaa hao wa watu waliopotea.
Kero la jamaa hao limekuja baada ya waziri mkuu wa Malaysia, Najib
Razak kusema udadisi wa data ya Satelite ulionyesha kuwa safari ya ndege
hiyo iliishia baharini Kusini mwa Australia.
Serikali ya China imeomba kuona data hiyo ambayo Malaysia imeamini kiasi cha kutoa msimamo wake.
Shughulii ya kuitafuta ndege hiyo MH370 imesitishwa kutokana na mawimbi makali baharini.
Mataifa mbali mbali yalijitolea kusaidia Malaysia kuitafuta nmdege
hiyo, juhudi ambazo zililengwa zaidi katika bahari ya Kusini Magharibi
mwa mji wa Australia Perth
Ndege hiyo MH370 ilipotea tarehe nane mwezi Machi, ilipokuwa njiani kuelekea Beijing kutoka Kuala Lumpur.
Ilikuwa imebeba abiria 239 ikiwemo raia 153 wa China.
Maandamano ya umma ni haramu nchini China,lakini hadi kufikia watu
hawa wakapanga maandamano kama hayo ni ishara kuwa hawana kilichobakia
kuwapa matumaini kabisa.
0 comments:
Chapisha Maoni