Kesi dhidi ya wafuasi 700 wa aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Mohammed Morsi, imeanza kusikilizwa mjini Cairo.
Miasaba hao ambao pia ni wafuasi wa chama kilichopigwa marufuku cha
Muslim Brotherhhood, wanakabiliwa na tuhuma za kufanya maandamano
yaliyozua ghasia mwaka jana.
Miongoni mwa watuhumiwa ni kiongozi wa vuguvugu hilo, Mohamed Badie.
Maafisa wa utawala wanaseama kuwa Badie hatafikishwa mahakamani leo kutokana na sababu za kiusalama.
Kesi hiyo inaendeshwa bila ya watuhumiwa wengi kupo mahakamani.
Ni watu 60 pekee waliokuwa mahakamani siku ya Jumatatu ambapo zaidi ya watuhumiwa wengine miatano walihukumiwa kifo.
Wengi Nchini Misri wamelaani hukumu hiyo.
Walihukumiwa baada ya kupatikana na hatia kwa mashitaka kadhaa
ikiwemo kumuua afisa wa polisi baada ya kuzuka ghasia mnamo Agosti
katika makabiliano na maafisa wa usalama, wakipinga kupinduliwa kwa
Mohammed Morsi.
Mawakili wao wanasema hawakuwa na nafasi ya kujitetea.
0 comments:
Chapisha Maoni